Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa leo Agosti 10, 2022 amefungua Mkutano Mkuu wa 44 wa kawaida wa CAF katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) Arusha.
Mkutano huo umehudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Patrick Motsepe.
Mkutano huo pia umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiongozwa na Waziri Mhe. Mohamed Mchengerwa, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi na Naibu Katibu Mkuu Said Yakubu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.