• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWATAKA MAWAZIRI WA MICHEZO KANDA YA 4 AFRIKA KIKUZA MICHEZO

Posted on: May 4th, 2023


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri wa michezo wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya Nne kuweka nguvu katika kuhakikisha wanakuza na kuendeleza michezo kwa Ukanda huo.

Amesema hayo leo Alhamisi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Michezo wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV Jijini Arusha.

Amesema kuwa mawaziri hao wawekeze kwenye kujenga uwezo wa kitalaamu ili kuzalisha wanamichezo wanaoweza kuleta mageuzi kwenye Sekta ya Maendeleo ya Michezo na Maendeleo kupitia Michezo.

 “Tusikubali kushika mkia kila siku na wala tusikubali kurudi nyuma”.

Amesema kuwa lengo la kila taifa ni kuona timu yake inashinda makombe ya Kimataifa hasa Kombe la Dunia.

“Tukiamua kuwekeza kwenye miundombinu ya michezo na ujuzi pamoja na kushirikiana tunaweza kufikia malengo makubwa kwenye sekta ya michezo”

“Tunapaswa kufika mahali pa kuona kuwa Tanzania ikishinda wote tumeshinda, Uganda ikishinda, wote tumeshinda, Ethiopia ikishinda wote tumeshinda. Tushirikiane ili tuwe mfano na kielekezo kwa Kanda nyingine za Mabaraza ya Michezo ya Umoja wa Afrika”.

Katika Hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wajumbe wa mkutano huo kuichagua Tanzania kuwa makao makuu ya Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Ukanda wa IV.

Amewaeleza wajumbe hao kuwa Tanzania ina kila sababu ya kupigiwa kura ya ndiyo kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuipa hadhi sekta ya michezo nchini.

Amesema kuwa uwepo wa mageuzi makubwa katika diplomasia ya michezo ya kimataifa ambapo chini ya uongozi thabiti wa Serikali, timu za Taifa za Tanzania na vilabu zinafanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa jambo hili linatia hamasa kwa wanachama kuona kuwa Tanzania inapiga hatua katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.

“Uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali kwenye Miundombinu ya Michezo ikiwemo ujenzi wa Viwanja Vikubwa na vizuri vya Michezo vinavyokidhi viwango vya Kimataifa vya CAF na FIFA. Mathalan, Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa ambao hutumiwa kwa Michezo ya Kitaifa na Kimataifa  ikiwemo Timu ya Taifa ya Brazili na Klabu ya Everton ambazo pia zimewahi kuutumia”

Katika Mkutano huo, Rais Dkt. Samia Aliwasilisha ujumbe maalumu kwa wajumbe na Mawaziri wa michezo wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya Nne kuichagua Tanzania kuwa makao makuu ya Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Ukanda wa IV.

 “Niwahakikishie kuwa Tanzania inauzoefu wa kuwa makao makuu ya taasisi mbalimbali za kimataifa, na pia Tanzania ina miundombinu yote muhimu ambayo itaiwezesha baraza hilo kufanya kazi kwa ufanisi” Amesema Rais Samia.

Naye Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Balozi Dkt Pindi Chana amesema kuwa tasnia ya michezo ni kati ya sekta ambazo inatoa ajira kwa vijana wengi “sekta ya michezo kwenye nchi wanachama ilitunga sheria ili kuendeleza vipaji, michezo inaiunganisha Afrika kuwa moja”

Ameongeza kuwa wataendeleza mapitio ya sheria kanuni na taratibu ili kuendelea kuikuza sekta ya michezo kwa kuwa michezo ni biashara na chanzo cha uhakika cha ajira kwa vijana.

Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.