Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Mwigulu Nchemba amezitaka nchi za Afrika Mashariki kuendelea kuimarisha matumizi ya mfumo wa kidijitali wa Ununuzi wa Umma - NeST, sambamba na kuendelea kutoa elimu ya matumizi ya mfumo huo, ili kuongeza uwazi, kupata thamani halisi ya fedha pamoja na kurahisisha kazi ya Ununuzi kwa maendeleo endelevu.
Dkt. Mwigulu ameyasema hayo mkoani Arusha wakati akifunga Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma Nchi za Afrika Mashariki, kwenye Kituo cha Mikutano ya kimataifa Arusha, Septemba 12, 2024 na kuzishauri nchi hizo kuimarisha mfumo wa Ununuzi , kwa manufaa ya nchi zote ili kuchangia jitihada za viongozi wa nmataka Jumuiyayhiyo ili kuinua hali za kiuchumi za Taifa nz wananchi wake.
"Endeleeni kutoa elimu kwa Umma kwa kuwa Taasisi zote za Umma zinapaswa kufanya ununuzi kupitia mfumo wa NeST, ili kuhakikisha matakwa ya Sheria Mpya ya Ununuzi wa Umma, Sura Na. 410, yanazingatiwa na watu wote ili kuongeza uwazi, uwajibikaji, ushindani na thamani ya fedha zinazotumika katika shughuli husika". Amesema
Aidha, amezitaka Taasisi za Umma kutumia fursa hiyo kuinua uchumi wa Afrika Mashariki kwa kutengeneza mikakati endelevu ya kuendeleza mashirikiano baina ya nchi zote katika kutekeleza kazi za ununuzi na ugavi kupitia mifumo ya kielektroniki, na kusisitiza kuwa jambo hili linawezekana na litafanyika kwa ufanisi zaidi kupitia ziara za mafunzo kutoka nchi moja mwanachama kwa kubadilishana wataalamu na uzoefu.
“Nimefurahishwa na kauli mbiu ya jukwaa hili inayosisitiza 'Matumizi ya Kidigitali kwa ajili ya Ununuzi Endelevu katika Sekta ya Umma', ninapenda kuwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ipo mstari wa mbele kuhakikisha kauli mbiu hii inatekelezwa kwa vitendo na ndio maana tumeuzindua rasmi mfumo wa NeST ambao utaleta mapinduzi na uwazi katika sekta hii". Amesema Mwingulu.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi ya Umma, Dkt. Leonada Magika amesema, Tanzania itaendelea kurekebisha makosa madogo madogo yatakayojitokeza kwenye mfumo wa manunuzi wa kidijitali uliozinduliwa ili ulete ufanisi.
Hata hivyo Jukwaa la 17 la Ununuzi wa Umma mwaka 2025, limepangwa kufanyika nchini Sudani Kusini, ambapo wamekabidhiwa zawadi kama ishara ya kukabidhiwa kijiti na nchi wenyeji Tanzania.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.