Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayofanya kazi kwa misaada ya wafadhili, yametakiwa kuweka wazi mapato na matumizi ya fedha zake.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Iddi Hassan Kimanta alipokuwa akizindua mpango wa shughuli mbalimbali wa miaka 40 ya shirika la World Vision Mkoani Arusha.
Amesema, mashirika hayo yamebeba jina la nchi hivyo wakiwa wawazi ndivyo nchi itapata sifa nzuri na wao watajenga uwaminifu kwa wafadhili wao.
Aidha, amewataka watumishi wa shirika la World Vision kusimamia miradi ya shirika hilo kwa uwaminifu ili shirika hilo liweze kutekeleza miradi mingi kwa maendeleo ya nchi.
Shirika la World Vision Tanzania limetimiza miaka 40 tokea kuanzishwa kwake mwaka 1981 na kilele cha maadhimisho hayo kinatarajiwa kufanyika Aprili 16,2021.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.