Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 umepitia jumla ya miradi 10 katika Wilaya ya Monduli nakuridhishwa na miradi yote.
Akizungumza katika hitimisho la ziara hiyo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bwana Abdalla Kaim ameipongeza Wilaya ya Monduli kwa kupata hati safi katika miradi yote iliyopitiwa na Mwenge Uhuru na kuwataka watekeleze maagizo yote yaliyotolewa na Mwenge huo kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo.
Mwenge wa Uhuru umepitia jumla ya miradi 10 ikiwemo ya Mazingira, afya, Miundombinu, shule, mradi wa uwezeshaji vijana kiuchumi,klabu ya rushwa iliyogharimu zaidi ya sh.bilion 1. Katika miradi hiyo,mradi 1 iliwekewa jiwe la msingi,mradi 1 ulifunguliwa, mradi 5 ulizinduliwa na miradi 3 ilitembelea.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekimbizwa katika Wilaya ya Monduli kwa umbali wa kilomita 171.2 na zinatarajia kumalizika katika Mkoa wa Arusha Julai 3,2023.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.