Wakuu wa idara wametakiwa kutowanyanyasa watalaamu waliopo katika idara zao bali wafanye nao kazi kwa ushirikiano na kwa kufuta haki na taratibu za utumishi wa umma.
Akitoa maelekezo hayo mkuu wa mkoa wa Arusha mheshimiwa Idd Kimanta alipokuwa akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya Longido, wilayani Longido.
Amesema atawalinda watumishi wote watakaotekeleza majukumu yao kwa ufasaa na wale watakaoshindwa hatakuwa na huruma nao kwani kila mtumishi ana wajibu wa kutekeleza majukumu yake kama alivyopangiwa.
Amesisitiza utendaji wao uzingatie nidhamu, upendo na ushirikiano ndio wataweza kuwahudumia wananchi kwa amani na bila kuwanyanyasa.
Nae, Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa Frank Mwaisombe amesema,yote yaliyozungumzwa na Mkuu wa Mkoa yamekuwa ya kuonya, kushauri na kuelekeza kwa watumishi hao.
Ameaidi kwa niaba ya watumishi wote kwenda kuyafanyia kazi maelekezo yote waliyopewa ili kujenga Longido iliyo bora na yenye maendeleo zaidi.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ameanza ziara yake ya kikazi katika wilaya zote za mkoa wa Arusha na ameanza na wilaya ya Longido kwa lengo la kujitambulisha kwa wananchi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.