Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi mkubwa wa maji katika Jiji la Arusha kwa gharama ya Shilingi Bilioni 520 utakapokamilika. Mradi huu pamoja na shughuli nyingine unahusisha uchimbaji wa visima virefu 56 na unatarajiwa kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Jiji la Arusha kwa zaidi ya asilimia 100 ikiwa ni pamoja na:
Kuongeza kiwango cha kuzalisha maji kutoka wastani wa lita 40,000,000 hadi lita 200,000,000 kwa siku.
Kuongeza idadi ya wakazi wanaopata maji kutoka wastani wa 325,000 hadi kufikia 600,000 wakiwemo wastani wa watu 250,000 wanaoingia na kutoka Jijini kila siku.
Kupunguza upotevu wa maji kutoka wastani wa asilimia 40 hadi asilimia 25.
Kuongeza mtandao wa maji safi kutoka asilimia 44 ya sasa hadi asilimia 100;
Kuongeza mtandao wa kukusanya majitaka kutoka asilimia 7.66 hadi asilimia 30
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.