Mkoa umeweza kuwaunganisha jumla ya wateja wapya 33,051 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ambayo ni sawa na 181.32% ya lengo la mwaka mzima la wateja 18,000. Jumla ya wateja 6,417 zikiwa ni taasisi, 210,306 makazi na 6,184 zikiwa ni sehemu za biashara zimewezwa kuunganishwa umeme hadi kufikia Machi, 2022.
Aidha, TANESCO ilisambaza umeme katika mitaa 30 ya Jiji la Arusha na mitaa 15 ya Arusha DC. Wamesambaza umeme kwenye maeneo 22 ya Arumeru, 12 Monduli, 23 Karatu, 9 Longido na maeneo 4 ya Ngorongoro. Aidha, jumla ya wateja 2,510 wameunganishiwa umeme kwa kipindi hiki kwa gharama ya shilingi bilioni 3,112,591,057.85.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.