Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha bwana David Lyamongi amewataka wadau wote wanashughulika na biashara ya madawa, vifaa tiba na vifaa tenganishi kutumia mazingira bora ya biashara na watalaamu waliobobea ili kulinda Afya za wananchi.
Bwana Lyamongi ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao kazi cha, wauzaji wa madawa, vifaa tiba na tenganishi kutoka Mkoa wa Arusha, kilichoandaliwa na Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA).
Vilevile ametoa onyo kali kwa wale wote wanauza dawa kwenye magari kwani hawafuati taratibu, kanuni na Sheria za madawa na hivyo kuhatarisha Afya na uhai wa watu hivyo wachukuliwe hatua kali dhidi yao.
Pia,ameitaka mamlaka ya dawa na vifaa tiba kuwachukulia hatua kali wale wote wanakiuka Sheria,kanuni na taratibu za madawa na vifaa tiba.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Vones Uwiso ameitaka mamlaka ya madawa na vifaa tiba kuendelea kutoa elimu zaidi katika Jamii ili kukuza ufahamu.
Aidha amewataka waongeze nguvu zaidi katika usimamizi ili kulinda Afya za wananchi.
Meneja wa Kanda mamlaka ya madawa na vifaa tiba bwana Proches Patric, amesema swala la kumlinda mwananchi linatakiwa litoke ndani ya Moyo wa mtu.
Mamlaka ya madawa na vifaa tiba Kanda ya Kaskazini imefanya kikao na wadau wa madawa, vifaa tiba na vifaa tenganishi ili kufafanua zaidi juu ya Sheria, kanuni na taratibu za ufanyaji kazi katika sekta hiyo.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa