Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amezitaka Halmashauri zote nchini zinazokusanya mapato zaidi ya shilingi Bilioni 5 kuhakikisha zinatenga fedha kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwenye halmashauri husika.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo jijini Mbeya wakati akizindua Bodi ya Ushauri ya TARURA tarehe 27.07.2024.
Amesema tangu TARURA ilipoanzishwa mwaka 2017 Halmashauri nyingi zimeacha kabisa kutenge fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara unakuta barabara za kwenye mitaa zina mashimo na zingine zinahitaji marekebisho kidogo tu ni mpaka wasubiri TARURa waje kufanya wakati wana mapato ya kutosha kuweza kurekebisha hizo changamoto.
Sasa kuanzia sasa nataka kuona Halmashauro zenye mapato zaidi ya Bilioni 5 zinatenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara na hata kujenga barabara za mitaani au vijijini kutegemeana na hadhi ya halmashauri.
Pia Mhe. Mchengerwa amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mitaa katika Jiji hilo.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa