Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha, wameendelea kuridhishwa na utekelezaji wa mradi wa jengo jumuifu la wagonjwa wa nje (OPD Complex), Kituo cha afya Levolosi, halmashauri ya Jiji, wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika sekta ya Afya jiji la Arusha leo Februari 26, 2024
Wakipokea maelezo ya utekelezaji wa ujenzi wa Mradi huo, unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 642, huku milioni 500 fedha toka Serikali Kuu na milioni 142 zikiwa ni fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya JJij, wamepongeza hatua za uyekelezaji wa mradi huo na kushauri kuongeza kasi ili mradi ukamilike na uanze kuwahudumia wananchi kama yalivyo malengo ya serikali.
Hata hivyo, lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuboresha miundo mbinu ya afya ili kuimairisha utoaji huduma za afya katika Halmashauri ya Jiji.
Kukamilika kwa mradi huo, licha ya kusogeza huduma za Afya karibu na wananchi, utarahisisha hali ya upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa wa nje, kurahisisha utunzaji wa kumbukumbu za wagonjwa na mawasiliano ya ndani kati ya watoa huduma kwa njia ya kielektroniki.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa