Na Elinipa Lupembe.
Makatibu wa Afya Nchini, wameamua kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Programu ya Kuhamasisha Utalii kwa kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro, mara baada ya kukamilisha mkutano wao wa mwaka 2024, uliofanyika kwa siku 5 mkoani Arusha
Makatibu hao wa Afya, wametembelea Hifadhi hiyo ya Ngorongoro mara baada ya kukamilisha Utalii wa Mkutano Arusha na kukamilisha kwa utalii wa maliasili, lengo likiwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayohamasisha Utalii
Katibu Mkuu wa (AHAST) Frank Omolo, amesema kundi hilo la Makatibu wa Afya, limeamua kutumia sehemu ya Mkutano wao wa mwaka 2024 kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro licha ya kuwa ni sehemu ya burudani kwao, wamefurahishwa kwa kuwa sehemu ya kuchangia pato la Taifa kupitia Utalii.
"Tumeshuhudia namna gani nchi yetu inavivutio vya asili ambavyo huwezi kupata sehemu nyingine duniani, niwahamasishe watanzania kujivunia nchi yetu kwa kutembelea vivutio vyetu ikiwa ni sehemu ya kuchangiq pato la Taifa letu lakini zaidi kumuunga mkono juhudi za Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan" Amesisitiza Okolo.
Hata hivyo Makatibu hao wa Afya wamevutiwa na safari yao ya kitalii kwenye hifadhi hiyo huku wakisisitiza kupata uelewa mkubwa na kuhaidi kwenda kuhamasisha wengine kutembelea Hifadhi hiyo na vivutio vingine vya Utalii vinavyopatikana nchini
Doris Mponela Katibu wa Afya Mbeya, amebainisha kufurahia muda wake kutembelea Hifadhini na kukiri akili yake kupata pumziko huku akiahidi kurudi ofisini kwake na kuhalasisha watumishi na watanzania wengine kufanya Utalii wa Ndania kA kutembele vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania
Mkutano wa Chama cha Makatibu wa Afya Tanzania mwaka 2024, umefanyika mkoani Arusha kwa siku tano wenye lengo la kujengeana uwezo na kubadilishana uzoefu wa kazi.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa