Ameyasema hayo alipokuwa akizindua Hoteli yenye hadhi ya nyota 5 ya Gran Melia iliyopo Jijini Arusha.
" Kutokana na hatua tuliochukua ya kutoa chanjo ya UVIKO 19 katika nchi yetu, hatua hii imepelekea kuwekwa miongoni mwa nchi chache zinazoendelea kupambana dhidi ya ugonjwa huu".
Serikali itaendelea kuhakikisha wawekezaji wanawekewa mazingira mazuri nayakuvutia ili waweze kuwekeza kwa wingi katika nyanja mbalimbali.
Amewashukuru wawekezaji wa hotel hiyo kwa kukubali kuja kuwekeza katika nchi yetu kwani wameweza kuwekaza kwenye zaidi ya Hoteli 5 ndani ya Tanzania na hivyo kutengeneza ajira nyingi kwa watanzania.
Kuwepo kwa Hoteli hiyo Mkoani Arusha itakuwa ni moja ya kichocheo cha kukuza Utalii ambao ulishuka kwa 59% kati ya mwaka 2019 na 2020 kutokana na janga la ugonjwa wa UVIKO 19.
Hivyo Serikali inaendelea kuhakikisha sekta hiyo ya Utalii inakuwa tena kwa kuwakaribisha wawekezaji zaidi na kuwawekea mazingira rafiki ya uwekezaji kwani ni moja ya sekta inayoingizia Serikali mapato makubwa.
Kutokana na uwekezaji uliofanywa na Hoteli hiyo kwenye sekta ya Utalii ambayo inagusa kila sekta hivyo anatarajia Hoteli hiyo itasaidia kukugua uchumi wa nchi kupitia wakulima na wavuvi kwa kutumia zaidi bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi hasa vinywaji ili kuweza kukuza soko la bidhaa hizo na kukuza uchumi wa nchi.
Pia, amezitaka hoteli zote nchini kutumia zaidi vyakula vya kitanzania, ili kudumisha Utamaduni wa Kitanzania.
Waziri wa maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro amemshukuru Rais Samia kwa kuleta uhai mpya kwenye sekta ya Utalii kupitia juhudi anazozifanya za kuitangaza nchi nje ya nchi, kuleta chanjo ya UVIKO 19 na kuleta ndege 2 upande wa Zanzibar vimekuwa ni miongoni mwa vichochea vya kukuza Utalii nchini.
Amesema kati ya Januari hadi septemba,2021 Utalii umekuwa kwa asilimia 248 na kuipatia nchi pato kwa asilimia 69 kati ya mwezi Januari na Octoba, 2021ukilinganisha na mwaka uliopita.
Nae, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amesema takribani asilimia 80 ya watalii wanaoingia nchini hufika Mkoa wa Arusha katika mbuga mbalimbali za wanyama na vituo vingine vya Utalii.
Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta chanjo ya UVIKO 19 katika nchi yetu ambayo imeleta hamasa kubwa katika sekta ya Utalii kwani watalii wengi wameweza kuamini nchi yetu ipo salama.
Mhe. Samia Suluhu Hassan amekamilisha ziara yake ya siku ya kwanza Mkoani Arusha kwa kuhudhuria sherehe za utoaji Kamisheni katika chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli na kuzindua rasmi Hoteli ya nyota 5 ya Gran Melia.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa