.Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa, ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari kata ya Seela Sing'isi, halmashauri ya Meru.
Katibu Tawala huyo, amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Meru, uongozi wa kukamilisha mradi huo kabla ya tarehe 10 Desemba, 2023, na kuahidi kurudi kukagua mara baada ya tarehe hiyo kufika.
"Ninakuagiza Mkurugenzi na timu yako, hakikisheni mradi huu, unakamilika kabla ya tarehe 10 Desemba, ukiwa na ubora unaozingatia thamani ya pesa, na kukiwa na samani zote zilizoelekezwa kwenye mradi". Amesisitiza Musa.
Akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Mkuu wa shule ya Sekondari Sing'isi, Mwl. Datus Muganga, amesema kuwa, mradi huo unatekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 584.2, kupitia mpango wa kuboresha Miundombinu ya Elimu Sekondari nchini (SEQUIP).
Ameongeza kuwa, mradi unajumuisha ujenzi wa Jengo la Utawala, vyumba 8 vya madarasa, Maabara tatu za masomo ya Sayansi, Maktaba, Chumba cha TEHAMA na matundu ya vyoo vya wavulana, wasichana na wenye mahitaji maalum, tanki la kuhifadhia maji na kichomea taka.
Awali, Ujenzi wa majengo ya shule za sekondari nchini, licha ya kuwa na mazingira rafiki na wezeshi yatakayopunguza kupunguza msongamano wa wanafunzi shuleni, zaidi ni maandalizi ya kupokea wanafunzi watakaopangiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2024
Ikumbukwe kuwa, uboreshaji wa miundombinu ya shule za serikali, ni utekelezaji wa Ilani ua chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 - 2025
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa