RC MAKONDA "KWA MAOMBI AU KWA DAWA NIA YANGU KILA MTU APONE"
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameweka wazi ni yake kwa wagonjwa kuwa, matamanio yake makubwa ni kuhakikisha kila mmoja anayefika anayekanyaga miguu yake kwenye Uwanja vya Sheikh Amri Abeid kwa ajili ya kupata huduma za matibabu anapona, iwe kwa maombi au kwa matibabu ili baadaye kila mwananchi awe na afya njema ya kuchangia uchumi wa familia na Taifa.
Mhe. Paul Christian Makonda ametoa yaliyoujaza moyo wake wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wanaoendelea kumiminika kwenye Kliniki ya Madaktari Bingwa na Wabobezi na kusisitiza kuwa hana nia nyingine yeyote tofauti na kuona kila mwananchi mwenye changamoto ya ugonjwa natibiwa na kupona na anakuwa na afya njema.
"Lengo letu sio idadi ya watu wengi, lengo letu sio kutaka umaarufu, lengo letu ni wananchi wahudumiwe vyema na wapate afya njema ili warejee katika maisha yao ya kupambania uchumi wa familia zao, ninaamini kwa maombi au kwa dawa watu watapona". Amebainisha Mhe. Makonda.
Hata hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa, ametangaza ujio wa Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumaini Nagu atakayeambatana na Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya afya ambao wanatarajiwa kuwa sehemu ya utoaji wa huduma za matibabu kwenye kambi hiyo inayotarajiwa kufikia kilele siku ya Jumapili ya Juni 30, 2024.
Kaulimbiu ya Kambi hiyo ya madaktari bingwa ni "Afya yako mtaji wako, kazi yetu ni kukupatia huduma bora"
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa