Na Elinipa Lupembe.
Wananchi wametahadharishwa kuwa makini na fomu wanazopewa na taasisi zinazokopesha fedha, kabla ya kuzisaini na kupewa mkopo
Rai hiyo, imetolewa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Mchemba, kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, kufungua rasmi Maadhimisho ya 3 ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayofanyika mkoani Arusha, kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Mhe. Mwigulu ameweka wazi kuwa, kumekuwa na kawaida ya watu, wanapohakikishiwa kupata mkopo, husaini fomu za mkopo, bila kusoma vizuri, masharti ya mikopo wanayoichukua na kuelewa vema kilicoandikwa kwenye mkataba huo, jambo ambalo limewaingiza watu wengi kwenye migogoro, pale wanapokwama au kushindwa kurejesha mikopo hiyo.
Amesistiza kuwa licha ya kwamba mikopo ni muhimunkatika amendeleo ya kiuchumi kwa mtu yoyote, ni vema kuchukua hatua kwa kusoma vizuri na kuelewa masharti ya mkopo kabla ya kusaini na kukopeshwa fedha na kuzitaka taasisi za kifedha kukaa na wateja wao na kuwaelewesha taratibu masharti ya mikopo kabla ya kuchukua.
"Watu wengi wakihakikishiwa kupata mkopo, huenda moja kwa moja kwenye jina na saini na kusaini fomu ya mkopo, bila kufahamu vema ,masharti ya mkopo, kupitia elimu inayotolewa hapa, tuanze kubadilika na kujifunza kusoma na kuelewa masharti ya mkopo, jambo ambalo litatoa fursa ya kufanya maamuzi sahihi.
Anamary James, amesema kuwa, mara nyingi fomu za mkopo huandikwa kwa lugha ya kiingereza jambo ambalo huwafanya wengi wao kushindwa kuelewa kilichoandikwa kutokana na kutokuifahamu lugha hiyo na kuomba fomu hizo kuandikwa kwa lugaha ya Kiswahili inayofahamika kwa watanzania wengi.
"Fomu za mkopo, zinaandikwa kingereza, sisi wajasiriamali hatujui kingereza, na tukifika kwenye mkopo, watalamu wanatuelezea mambo mepesi mepesi kumbe ndani, imendikwa masharti magumu ambayo bila kujua tunajikuta tusaini" Anamary
Jane Shayo,ameomba serikali kusimamia kubadili lugha kwenye fomu za mikopo na kuandikwa kwa lugha rahisi ya Kiswahili ili wakopaji, waweze kufanya maamuzi sahihi.
"Sisi wajasiriamali, hatushindwi kurejesha mikopo, kwa sababu tunafanya biashara, tatizo ni masharti magumu yanayoandikwa kwa Kingereza, lugha ambayo wengi wetu hatuifahamu vizuri, tunaomba serikali itusaidie, fomu za mkopo ziandikwe kwa lugha yetu ya Kiswahili" Amesema Jane.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha, ni “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya UUchumi
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa