Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddi Hassan Kimanta ameitaka bodi ya manunuzi na ugavi kuwachukulia hatua kali wataalamu wa manunuzi na ugavi pindi watakapokiuka taratibu na sheria za taaluma yao.
Ameyasema hayo alipokuwa akifunga kongamano la 11 la wataalamu wa manunuzi na ugavu,jijini Arusha.
“Ifike wakati sasa hawa wataalamu wetu wa manunuzi na ugavi wachuliwe hatua kali za kisheria pindi wanapoenda kinyume na sheria na taratibu za manunuzi”.
Amewataka wakazingatie sheria na taratibu za manunuzi serikalini na kufanya kazi kwa nidhani ili kuhakikisha miradi yote ya maendeleo ambayo serikali inatoa fedha zake inakamilika kwa wakati na kwa ubora wa juu.
Kimanta amewasisitiza wakaonyane wao kwa wao pindi makosa yanapokuwa yamefanyika na pia kuwatolea taarifa wale wote ambo watakuwa wanafanya kazi bila ya kusajiriwa na bodi yao.
Aidha, amewataka wataalamu hao watumie kongamano hilo kama sehemu ya kujijengea uwelewa wa mambo mbalimbali yanayohusu taaluma yao.
Kongamano la wataalamu wa manunuzi na ugavi limefanyika kwa siku 3 jijini Arusha na kuwakutanisha watalaamu wa manunuzi na ugavi wa serikalini kutoka nchi nzima.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa