Watengaji wote wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kuwa karibu na miradi ya maendeleo wanayoitekeleza katika maeneo yao.
Akitoa maelekezo hayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Idd Kimanta, amesema kuna baadhi ya miradi ya maendeleo katika halmashauri ya Ngorongoro kasi yake ya utekelezaji bado ipo chini.
“Sijaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo katika halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro japo kwa asilimia kubwa miradi mingi imetekelezwa vizuri sana”.
Amewataka wawe watendaji makini hususani katika kusimamia miradi ya maendeleo ili waweze kwenda sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano.
Kimanta amesisitiza zaidi kuwa hataweza kuwasamehe watendaji wote watakaoshindwa kusimamia vizuri miradi hiyo.
Amewataka wataalamu wasimamie miradi yote katika maeneo yao hata kama fedha zake zimetolewa na serikali au ni nguvu za wananchi.
Amesema hatavumilia kuona miradi inakwama watalaamu wapo na hawasimamii.
Mheshimiwa Kimanta amefanya ziara ya kikazi katika wilaya hiyo ambapo alikagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara kwenye maeneo mbalimbali.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa