Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluh Hassan amewasili Mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu na Viongozi wengine wa Chama na Serikali, kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro, asubuhi ya leo Jumamosi Machi 08, 2025.
Mhe. Rais yupo Mkoani Arusha kuongoza Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika Kitaifa mkoani humo, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Kauli Mbiu: Wanawake na Wasichana 2025; Tuimarisha Haki, Usawa na Uwezeshaji
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa