Halmashauri za Mkoa wa Arusha zimetakiwa kwenda kusimamia mapato katika maeneo yao, ili fedha hizo zikaisaidie serikali katika kuboresha huduma mbalimbali za maendeleo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Iddi Hassan Kimanta alipokuwa akifungua kikao cha ushauri cha Mkoa (RCC) kwa mwaka 2020/2021.
Amesema kuzembea kukusanya mapato ni kuikwamisha serikali katika kuleta miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi na baadhi ya huduma kukosekana.
Kimanta amesesisitiza kuwa mapato hayo yanasaidia sana katika kuongeza kiasi cha dawa katika hospitali zetu,kuboresha miundombinu ya barabara na huduma nyingine nyingi.
Aidha, ameziagiza mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kushirikiana katika kukusanya kodi katika maeneo yote ambayo yanatakiwa kulipa kodi.
Amesema kulipa kodi ni jukumu la kila anaetakiwa kulipa na hii ndio kuonesha uzalendo kwa serikali yetu ambayo inapambana kuhakikisha kila Mtanzania anayaona na kufurahia maendeleo ya nchi yao.
Mkoa wa Arusha katika kuhakikisha maendeleo yanaletwa kwa kasi kubwa, imependekeza bajeti ya kiasi cha bilioni 303 kwa mwaka 2021/2022 kwa matumizi ya kawaida na mipango ya maendeleo katika Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Sanduku la Barua: 3050 Arusha
Simu: 27 254 5608
Simu Nyingine: 027 254 4950
Barua Pepe: ras@arusha.go.tz
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa