Sera ya Nishati ya Taifa ya Mwaka 2015, pamoja na mambo mengine inaweka mkazo kuhusu kuongeza uzalishaji wa umeme ili kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na huduma hiyo. Sanjari na Sera hiyo, vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano ni pamoja na kuendelea kusambaza umeme wenye uhakika mijini na vijijini na kuongeza kiwango cha uunganishaji wa umeme kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA).
Katika Mkoa wa Arusha, jumla ya 5,621 na vijiji 90 vinatarajiwa kuunganishwa na umeme wa REA ifikapo mwaka 2020. Kufikia mwezi Juni 2019 jumla ya vijiji 41, kati ya 90, na kaya 1,090 zilikuwa zimeunganishwa. Kwa ujumla utekelezaji wa Mradi wa umeme vijijini katika Mkoa wa Arusha umefikia asilimia 43 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2019.