MAJUKUMU YA SEKSHENI YA HUDUMA YA URATIBU NA USIMAMIZI WA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA:
Kushauri na kusimamia matumizi bora ya rasilimali fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
Kukuza na Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutekeleza utawala bora;
Kuwezesha mapitio ya muundo na michakato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
Kushiriki katika kaguzi za kawaida/kushtukiza zinazohusu utendaji kazi na majukumu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa;
Kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuandaa bajeti na matumizi;
Kuratibu na kushauri Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusiana na masuala ya kiutumishi (kuajiri, kujaza nafasi wazi, masuala ya kinidhamu, kupandisha madaraja n.k);
Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusiana na masuala yoyote kiutumishi;
Kuratibu, kuandaa, kutekeleza, usimamizi na ufuatiliaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusiana na mkataba wa huduma kwa mteja;
Kumshauri Katibu Tawala Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika utekelezaji wa sheria za kazi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Sanduku la Barua: 3050 Arusha
Simu: 27 254 5608
Simu Nyingine: 027 254 4950
Barua Pepe: ras@arusha.go.tz
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa