Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia amemuondolea majukumu ya usimamizi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari Umoja, bwana Fred Lubida.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Dkt. Kihamia kukagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Wilaya ya Arumeru na kutorishishwa na kasi ya ujenzi wa chumba cha darasa katika shule hiyo.
"Kwa kuwa Mwalimu Mkuu amesema bado yupo kwenye hatua ya kujifunza maswala ya ujenzi basi atupishe kwanza achaguliwe Mwalimu mwingine mwenye uzoefu asimamie ujenzi huu ili muweze kwenda na kasi ya Serikali ya awamu ya sita",alisema.
Ametoa wito kwa wakuu wa Shule zote za Sekondari Mkoa wa Arusha kuhakikisha wanasimamia vyema ujenzi wa Madarasa katika shule zao na ujenzi ukamilike ifikapo Disemba 5,2021.
Serikali imetoa jumla ya Bilioni 1.4 fedha za mapambano dhidi ya UVIKO 19 kwa Halmashauri ya Meru kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 70.
Hivyo amewataka viongozi wa Halmashauri kusimamia fedha hizo kwa umakini ili ziweze kukamilisha malengo yaliyowekwa ya ujenzi wa Madara yote 70.
Nae, Mkurugenzi wa halmshauri hiyo Mwl. Zainabu Makwinya amewataka mafundi ujenzi kuongeza idadi ya vibarua kwani itawasaidia kufanya kazi kwa muda mfupi zaidi huku gharama ikibaki pale pale.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa