Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Tanga imesema inasogeza huduma zake karibu na wateja wake wa Mkoa wa Arusha kwa kujenga bandari kavu maeneo ya King’ori.
Akisoma taarifa ya maendeleo ya bandari ya Tanga kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha msimamizi wa bandari hiyo bwana Percival Ntetema,amesema huduma za bandari ya Tanga zimeimarika sana kwa sasa na bandari hiyo inaongoza kwa kutoa mizigo haraka kwa upande wa Afrika Mashariki.
Amesema ilikuongeza ufanisi zaidi Bandari ya Tanga itashirikiana na mamlaka ya Reli Tanzania kufufua reli ya Tanga hadi Arusha ili kupanua wigo zaidi wa usafirishaji mizigo kwa wafanyabiashara wa Arusha na mikoa jirani.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya Bandari Tanzania ing. Deusdedit Kakoko amesema, mamlaka inaanzisha mtandao wa pamoja wa mawasiliano katika mamlaka na pia kutakuwa na mtandao wa nchi nzima wakusimamia makusanyo ya mapato kwa taasis husika.
Kakoko amesema hali hii itasaidia kuondoa au kumaliza kabisa urasimu uliopo kwa sasa katika bandari za nchi hii na pia mtandao huu utamrahisisha mteja kufanya malipo kwa haraka na urahisi na hivyo kuokoa mda wa mizigo kukaa bandarini.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameishauri mamlaka ya Bandari Tanzania kuhakikisha inajitaidi kumaliza kero zinazotolewa na wateja wao hususani urasimu kwa kuanzisha mfumo wa makusanyo ya pamoja kwa taasis husika.
Mmlaka ya Bandari Tanzania imekutana na kufanya kikao na baadhi ya wafanyabiashara kutoka Mkoa wa Arusha kwa lengo la kusikiliza na kuchukua maoni ya namna ya kuboresha huduma katika bandari za Tanzania. a
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa