Makonda amesema kutakuwa na michezo kama mpira wa miguu, ukiwahusisha wachezaji wa kike kutokataadhimishwa Kitaifa mkoani humo Machi 8, 2025 itakuwa ya kitofauti kwa kuwa wameandaa matukio mbalimbali.
Mhe. Makonda amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha tano cha Serikali mtandao, kinachofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), ambapo mgeni rasmi ni Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.
Amesema kutakuwa na siku saba ambapo mambo mbalimbali yatafanyika na tukio hilo limepewa jina la 'Wiki ya Wanawake'.
“Sherehe ya Siku ya Wanawake Kitaifa Arusha tunafanya kitu cha tofauti, haitakuwa tu tarehe 8 kama ilivyozoeleka. Mkoa wa Arusha tumekubaliana kuanza sherehe zetu tarehe 1 Machi, ambapo tutakuwa na siku saba za Wiki ya Mwanamke. Tumeomba wizara nane, na kazi ya kwanza itakuwa kutoa huduma,” amesema Makonda
Ametaja huduma zitakazotolewa ndani ya siku hizo saba kuwa ni pamoja zile za afya, huduma za kisheria na
huduma ya elimu ya fedha.
Pia, Mhe. Makonda amesema kutakuwa na michezo kama mpira wa miguu, ukiwahusisha wachezaji wa kike kutoka timu za Simba Queens, Yanga Queens, JKT Queens na Fountain Gate FC.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa