Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kupitia kampuni yake ya Usafi na Unyunyiziaji dawa (SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co. Ltd) wameingia makubaliano na Jiji la Arusha ili kufanya usafii kwenye viunga vya Jiji hilo ili kuhakikisha kuwa Jiji na Mkoa mzima wa Arusha unasalia katika hali ya usafi na hivyo kuvutia zaidi wageni na watalii wanaodhuru mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda,wakati wa ufanyaji Usafi kwenye Jiji la Arusha leo Jumanne, amewaambia wakazi wa Arusha kuwa katika makubaliano hayo, Mwananchi atakayebainika kutupa taka hovyo atatozwa faini ya Shilingi Milioni moja, akiwataka wananchi wenye tabia ya kutupa taka hovyo kuchukua tahadhari dhidi ya utekelezaji wa sheria na kanuni hiyo ya usafi wa Jiji la Arusha.
Katika Hatua nyingine, Mhe. Makonda pia amewahimiza wananchi wa Arusha kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha katika jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanayoikumba dunia nzima kwasasa kutokana na ukataji miti hovyo na shughuli nyingine za kibinadamu.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa