Jamii ya Watanzania imetakiwa kubadili Mtindo wa maisha usiofaa ili kujenga Afya bora na kuleta tija kwa Taifa letu.
Yamesemwa hayo na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha bwana Hargeney Chitukulo alipokuwa akifungua huduma za afya katika maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza katika kiwanja cha sheikh Amri Abeid,Jijini Arusha
Amesema Jamii inapaswa kuzingatia ulaji unaofaa kwa kula mlo kamili, Matunda na mbogamboga zakutoka.
Aidha amesisitiza Jamii inapaswa kuepuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi,chumvi nyingi, vinywaji vyenye sukali na kilevi
Njia zitakazo ifanya Jamii kuepuka magonjwa yasiyoambukiza ni kama vile;kufanya mazoezi ya mwili na kuepuka msongo wa mawazo.
Kufanya uchunguzi wa Afya angalau mara moja kwa mwaka hasa kwa wenye umri zaidi ya miaka 40.
Akisisitiza zaidi, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu bwana Kasper Mmuya amesema magonjwa haya yanatukumba ni kwasababu hatuna tabia ya kupima mara mara hivyo kushindwa kuyazuia.
Ni dhahiri kwamba Jamii yetu inabidi ijenge tabia ya kupima afya zetu mara kwa mara ili kuweza kuyadhibiti magonjwa haya yasiyoambukiza
Maadhimisho hayo ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza yameanza mnamo Novemba 6,2021 na yanatarajiwa kufungwa Novemba 13, na Mhe. Dorothy Gwajima, Jijini Arusha.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa