"Kazalisheni bidhaa zenye ubora mzuri ili muweze kupata masoko ya nje ya nchi kirahisi".
Maagizo hayo ameyatoa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha bwana David Lyamongi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella alipokuwa akifunga mkutano wa kwanza wa chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kilichofanyika Jijini Arusha.
Dunia kwa sasa imefunguka katika masoko ni soko huria ndio tunalo, hivyo Tanzania ili tuweze kutambulika Kimataifa ni lazima bidhaa zetu ziwe bora naza kuvutia ili kuleta ushindani wenye tija.
Hivyo changamkieni soko hili ili mkue katika biashara na kutambulika zaidi kwani serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa