Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainab Katimba, amesema Serikali imetenga fedha nyingi zinazotumika kuanzisha miradi yenye gharama kubwa na ya kimkakati kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Taifa. Ni katika muktadha huo, amewasihi wananchi katika Uchaguzi wa Serekali za Mitaa Novemba 27, wachagua viongozi watakaokwenda sambamba na kasi, ubora, na nia ya dhati ya Rais Samia Suluhu Hassan ili kuboresha na kulinda miradi hiyo.
Zainab ametoa wito huo wakati wa hafla ya utiwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Soko Kuu katika eneo la Mwanga na Soko la Samaki katika eneo la Katonga, iliyofanyika katika Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.
Amewasihi wananchi kuchagua viongozi wenye uadilifu, uaminifu, na uzalendo, ambao wataweza kusimamia miradi yote iliyoanzishwa na Serikali kwa manufaa ya umma, na kuepuka kuchagua viongozi ambao lengo lao ni kuvuruga, kukwamisha, au kujinufaisha binafsi.
✍️ @marikiadrina
#tbconline #tbcupdates #tbcdigital
#tbconline #tbcupdates #tbcdigital
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa