Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, akizungumza na Maelfu ya wanawake mkoa wa Arusha, wameliojitokeza kwenye Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ngarenaro,Jijini Arusha.
Mhe. Emmanuela amewapongeza wanawake hao kwa kushiriki katika siku hiyo Maalum kwa wanawake wote Duniani, siku ambayo imeleta mwamko mkubwa kwa wanawake kwa kuwafanya kuwa wajasiri, kuungana kwa nguvu moja, kuinuana jambo ambalo limeleta mafanikio makubwa kwa wanawake wengi nchini.
Aidha, amewataka wanawake kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali yao ya awamu ya sita chini ya uongozi mahiri wa Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amabyo imatekeleza miradi mingi ya maendeleo inayomguza mwananmke moja kwa moja ikiwemo ujenzi wa shule na utoaji wa elimu bila malipo, uwepo wa vituo vya kutolea huduma za afya wenye lengo la kuondoa vifo vya wananwake na watoto wakati wa kujifungua, na kuongeza kuwa juhudi hizo za Serikali zinapaswa kuungwa mkono.
Ameongeza Kuwa, Serikali imeendelea kusimamia sera za kuwakomboa na kuwainua wanawake kijamii na kiuchumi, kwa kuwajengea uwezo pamoja na kuwawezesha kuunda vikundi vya kuweka na kuwekeza na kuanziasha biashara ndogondogo na kupata mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa na Mamlakala za Serikali za Mitaa.
Kauli Mbiu ni "Wekeza kwa Mwanawake ili Kuharakisha Maendeleo ya Taifa Pamoja na Ustawi wa Jamii"
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa