Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.John V.K Mongella, amemuapisha Mkuu mpya wa wilaya ya Monduli, Mhe. Festo Shemu Kiswaga asubuhi ya leo, hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha.
Mhe. Festo Kiswaga amekula kiapo cha Kuitumikia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nafasi hiyo ya ukuu wa wilaya kwa mujibu wa Sheria ikiwa ni pamoja na Kuhifadhi, Kuilinda na Kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Kiswaga mara baada ya kuapishwa, amemshukuru Mungu kupitia Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kuwatumikia wananchi wa Monduli.
Aidha, ameahidi kufanya kazi kwa bidii kwa kushirikiana na wananchi, viongozi na watalamu wote wa Monduli na Mkoa, ili kuhakikisha wananchi wa Monduli, wanapata huduma kama inavyoelekezwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa.
"Ninaahidi kufanya kazi kwa bidii kwa utumishi uliotukuka katika mkoa wa Arusha, chini ya kiongozi shupavu wa mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, kwa kufanikisha haya, ninaomba ushirikiano kutoka kwenu, uongozi wa chama, Kamati za Usalama, wananchi na watalamu wote ili kufikia malengo ya Serikali" Ameweka wazi Mhe.Kiswaga
Awali Mhe. Festo Kiswaga, aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, mwishoni mwa wiki iliyopita, Machi 09, 2024.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa