Mkoa wa Arusha, umepambwa Mafataki yaliyopigwa kitalamu na yakionekana angani kwa rangi mbalimbali zenye kuchora maua mazuri kwenye maeneo matano ya Jiji la Arusha, lengo ikiwa si maadhimisho tu bali kuipa heshima Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki (EAC) iliyotimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake kwa awamu ya pili mwaka 2000.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Paul Makonda Makonda Rc Paul , ametimiza ahadi hiyo ya kupiga mafataki, aliyoitoa
wakati akifungua hafla ya Usiku wa Nyama Choma Arusha na Maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki, iliyofanyika mkoani humo usiku wa kuamkia Novemba 25, 2024.
"Itakapofika saa nne kamili usiku tukio la kupigwa kwa Fataki litafanyika kwenye maeneo matano tofauti, ikiwa ni ishara ya kuipa heshima Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki huku wananchi wa nchi zote nane wakishuhudia tukio hilo". Amesema
Aidha, Maadhimisho ya miaka 25 ya kuundwa kwa Jumuiya hiyo ya Kikanda yatafuatiwa na Mkutano wa Jumuiya hiyo, utafanyika kwa siku mbili kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) na kuhudhuriwa na maraishi wa nchi zote nane za Jumuia huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan Samia Suluhu Kwanza akiwa Rais mwenyeji.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa