JAMII YA WAHDZABE WAJITOKEZA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA ORODHA YA WAPIGA KURA 2024.
Ikiwa zoezi la Uandikishaji wapiga kura katika daftari la wapiga Kura linahitimishwa leo Oktoba 20,2024 Jamii ya Wahadzabe pamoja na wadatoga wilayani karatu wamejitokeza kwa wingi Kujiandikisha katika Orodha hiyo ya wapiga kura ikiwa ni baada ya kufikiwa na kuhamasishwa kujiandikisha.
Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Bw. Juma Hokororo ambae ndiye amesimamia zoezi la kujiandikisha kwa wananchi hao amesema kujitokeza kwa wingi kwa jamii hiyo ni matunda ya hamasa na elimu waliyotoa kwa watu wa jamii hiyo kabla ya Zoezi la uandikishaji kuzinduliwa.
Amesema kumekua na changamoto ya watu wa jamii ya wahadzabe kusahaulika au kugoma kushiriki masuala muhimu ya kijamii kama uchaguzi lakini mwaka huu wamejotokeza kwa wingi jambo linalo ashiria kufikiwa kaa Malengo waliyojiwekea.
Aidha Wananchi hao jamii ya Wahadzabe wameishukuru serikali ya karatu na Tanzania kwa ujumla kwa kushirikishwa kwa karibu katika zoezi hilo muhimu kwa kila mwananchi wa taifa hili, wakiahidi kushiriki kikamilifu kwenye mchakato huo wa uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa