Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, amelipongeza Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, kwa kufanya kazi kwa weledi na kushirikisha jamii, jambo ambalo linazidi kuimarisha usalama wa mkoa wa Arusha, mkoa ambao shughuli ni kitovu cha Utalii nchini.
Mhe. Mongella ametoa pongezi hizo wakati wa sherehe za kuwapongeza Askari wa Jeshi la Polisi waliofanya kazi vizuri na waliostaafu utumushi wa Umma, mwaka 2023, zikiwa ni sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2024, zilizoandaliwa na Jeshi hilo mko wa Arusha na kufanyika kwenye hoteli ya Primier eneo la Sakina Wilaya ya Arumeru.
Amethibitisha kuwa, hali ya utulivu na amani ya mkoa wa Arusha, ni matokeo ya kazi kubwa inayofanywa na Jeshi la Polisi kupitia dhana ya ulinzi shirikishi kati ya Jamii na Jeshi hilo, unaopelekea jamii kushiriki katika ulinzi na usalama inasababisha utulivu wa hali ya juu na kuifanya jamii kujikita lwenye shughuli za uzalishaji kwa maendeleo ya jamii na taifa.
"Serikali kupitia dhana ya ushirikishwaji wa jamii katika ulinzi na usalama, inaunganisha moja kwamoja na mchakato wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, amani ya mkoa wa Arusha inasababisha wananchi kufanya kazi na sio kupambana na migogoro isiyo ya lazima" Amsema Mhe. Mongella.
Ameongeza kuwa, Matunda ya Utalii mkoani Arusha yaliyochochewa na tamthilia ya Royal Tour iliyofanywa na Me. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yanachachushwa na Jeshi la Polisi kwa kuimarisha Ulinzi na Usalama kuhakikishia ulinzi wa watu na mali zao
Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi, ACP Justine Maseja, amesema kuwa ni desturi ya Jeshi hilo la Polisi, kukutana pamoja nje ya kazi walau mara moja kwa mwaka ili kuopongezana Askari Polisi, waliofanya vizuri kwa mwaka husika, kuwapongeza Askari
waliolitumikia Jeshi hilo na hatimaye Kustaafu kwa mujibu wa sheria pamoja na kubadilishana mawazo nje ya eneo la kazi.
"Kwa mwaka 2023 tunawapongewa Askari 30 waliofanya kazi vizuri na askari 39 walolitumikia Jeshi la Polisi na kustaafu kwa mujibu wa sheria mwaka 2023, tunatoa vyeti vya pongezi ikiwa ni ishara ya kuthamini kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kulitumikia Taifa kupitia Jeshi letu la Polisi" Ameweka wazi RPC.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa TATO Henry Kimambo, amesema kuwa, Sekta ya Utalii ina uhusiano mkubwa na Jeshi la Polisi, kutokana na ukweli kwamba, hulka ya watalii ni kutembelea maeneo ambayo kuna hali ya amani na utulivu
"Kabla mtalii hajafanya maamuzi ya kutembelea vivutio vya utalii, hutazama kwanza hali ya amani na utulivu wa nchi husika, mambo mengine hufuata baada ya kujihakikishia usalama, nchi yetu imeweka mipango imara kwa kuwa na ushirikiano kati ya sekta ya Utalii na Jeshi la Polisi" Amesema Kimambo
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa