• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

JUMUIYA YA WAHASIBU WAKUU AFRIKA WATAKIWA KUWEKA MIFUMO YA USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA.

Posted on: December 2nd, 2024

Na Elinipa Lupembe 



Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika  wametakiwa kuandaa mapendekezo na mikakati  madhubuti ya usimamizi wa fedha za Umma inayoweza kukabiliana na changamoto zinazojitokeza duniani ikiwa ni pamoja na athari za mabadiliko ya tabia nchi, mabadiliko ya kiteknolojia na mabadiliko ya kiuchumi. 



Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa Innocent L Bashungwa  wakati akifungua Mkutano wa Pili wa Mwaka wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (AAAG) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha mapema leo Desemba 02, 2024.



Mhe. Bashungwa amesisitiza kuwa, uwepo wa mifumo thabiti ya usimamizi wa fedha za Umma, utapunguza gharama za usimamizi, kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi wengi zaidi.



Aidha, ametoa wito kwa Jumuiya hiyo kupendekeza mbinu mpya za kuboresha usimamizi wa fedha za umma kupitia matumizi ya teknolojia ya kidijitali ili kuongeza ufanisi, uwazi na uwajibikaji.



"Niwatake wana Jumuiya  kuona namna ya kukuza ushirikiano wa karibu kati ya Serikali, Sekta Binafsi na Asasi za kiraia, katika usimamizi wa fedha za Umma hasa katika kutekeleza miradi ya maendeleo".Amesema



Naye Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ameeleza usimamizi madhubuti wa fedha unasaidia wananchi kujenga tabia ya kulipa kodi kwa hiari ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazofanya vizuri.



Mhe. Nchemba amethibitisha hayo kwa kutolea mifano ya miradi iliyokamilika na inayotekelezwa  nchini ikiwemo Bwawa la Kufua Umeme, miradi ya umwagiliaji, miundombinu ya barabara, ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi) pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR)



Hata hivyo, Mhasibu Mkuu wa Serikali wa Ufalme wa Lesotho na Mwenyekiti wa Jumuiya ya AAAG, Malehlonolo Mahase ameeleza kuwa,  kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo kuna malengo na manufaa muhimu katika usimamizi bora wa fedha za umma na kuimarisha utendaji katika nchi za Afrika.



Awali, Mkutano huo wa umebeba kauli mbiu ya “Kujenga Imani ya Umma katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Ukuaji Endelevu”.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa