Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 umepitia jumla ya miradi 9 katika Wilaya ya Karatu nakuridhishwa na miradi yote.
Akizungumza katika hitimisho la ziara hiyo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bwana Abdalla Kaim ameipongeza Wilaya ya Karatu kwa kupata hati safi katika miradi yote iliyopitiwa na Mwenge Uhuru na kuwataka watekeleze maagizo yote yaliyotolewa na Mwenge huo kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo.
Mwenge wa Uhuru umepitia jumla ya miradi 9 ikiwemo ya Mazingira, afya, Miundombinu, shule, mradi wa uwezeshaji vijana kiuchumi,klabu ya rushwa iliyogharimu zaidi ya sh.bilion 7. Katika miradi hiyo,mradi 1 uliwekewa jiwe la msingi,miradi 2 ulifunguliwa, mradi 3 ulizinduliwa na miradi 3 ilitembelea.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekimbizwa katika Wilaya ya Karatu kwa umbali wa kilomita 242.20 na zinatarajia kumalizika katika Mkoa wa Arusha Julai 3,2023 na kukabidhiwa katika Mkoa wa Mara Julai 4,2023.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa