Na.Elinipa Lupembe.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi - Taifa, Komredi Abdulrahamani Kinana amewataka watanzania kuyaenzi maisha ya Hayati Edward Lowassa kwa kuwa, wazalendo pamoja na kuuenzi umoja wa kitaifa kwa kushirikiana.
Kinana ameyasema hayo wakati akitoa Salamu kwenye Ibada maalum ya shukrani iliyoandaliwa na Familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Ngoyai Lowassa, na kuwataka watanzania kuayenzi maisha yake kwa kuchapa kazi.
Amesema kuwa, Edward Lowassa alikuwa ni mzalendo na mchapa kazi na mwenye kusimamia yale aliyoyaamini, yanamanufaa na zaidi kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla wake.
"Tunapohubiriwa suala la uchapakazi Lowassa ni darasa la uwajibikaji, kwa kuwa alikuwa kiongozi mzalendo kwa Taifa hili la Tanzania,aliyependa kujituma na kuwajibika kwa maslahi ya Taifa" Amesema Kinana
Aidha, amewataka watanzania wote kuendelea kuuenzi umoja wa kitaifa uliojengaka enzi na enzi kwa kushikamana bila kujali wala kuathiri tofauti za kiimani wala itikadi za kisiasa.
"Watanzani tuendelee kuimarisha undugu wetu kama watanzania huku tukiendelea kumtanguliza Mungu, kila mtu ana dini yake ila tunaamini Mungu mkoja, sisi ni wamoja tukimtegemea Mungu Nchi yetu itakuwa na Baraka". Amesema Kinana
Awali, familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Ngoyai Lowassa imeandaa ibaada ya shukrani, kwenye kanisa la KKKT Usharika Monduli, inaada iliyoongozwa na Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazin Kati, Mchungaji Lareton Loishiye.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa