Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainabu Katimba (Mb) amsema serikali imefanya maandalizi makubwa katika usimami wa mikopo ya 10% kwani imeamua kuanzisha kitengo maalumu cha usimamizi wa Mikopo hiyo kwa ngazi ya Wizara, na kamati ya usimamizi wa mikopo hiyo katikati ngazi ya Mikoa, Halmashauri na kata.
Mhe. Katimba amesema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Christina Christipher Mnzava alitakakujua Je Serikali imejipanga vipi katika usimamizi wa mikopo ya 10% pindi itakapoanza kutolewa tena kuanzia Julai moja?
“Timu iliundwa kufanya mapitio na kuhakikisha unatengenezwa utaratibu bora zaidi kwaajili ya kuhakikisha Mikopo hii inatoka na inaenda kuwanufaisha walengwa na tayari katika Muundo wa usimamizi wa mikopo hii kutaanzishwa Kitengo cha usimamizi wa Mikopo hii katika ngazi ya Wizara Ofisi ya Rais TAMISEMI na kamati za usimamzizi wa Mikopo hii katika ngazi ya Mikoa, Kalmashauri na Kata” Mhe. Katimba.
Amesma Mikopo hii ya asilimia kumi inayotokana na Mapato ya ndani ya Halmashuri ilisitishwa kutokana na maelekezo ya serikali ya kuangalia upya utaratibu na changamoto zilizokuwepo hapo awali katika utoaji wa mikopo hiyo.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa