Maafisa Elimu wa halmashauri zote za Mkoa wa Arusha wametakiwa, kuhakikisha kuwa wanafuatilia Wanafunzi wote waliopangiwa kujiunga na kidato cha kwanza ambao hawajaripoti wanaripoti na kuanza masomo kwenye shule waliopangiwa.
Akizungumza wakati akifungua kikao hicho, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Afisa Elimu mkoa wa Atusha Mwl. Abel Mtupwa, kikao kazi kilichowakutanishz Maafisa Elimu Msingi na Sekondari wa halmashauri, Wathibiti ubora wa shule, Makatibu wasaidizi wa TSC,Viongozi wa TAHOSSA,Wakuu wa shule na Maafisa Elimu kata, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Amewataka viongozi hao wa Elimu kwa nagzi zote, kuwafuatilia wanafunzi waliopangiwa kujiunga na Kidato cha kwanza na hawajaripiti,kuhakikisha wanapata taarifa zao na kama wamehamia shule nyingine ama la na kutoa taarifa zao.
"Serikali imeshafanya maandalizi yote ya kuhakikisha wanafunzi wanakua shuleni kwa wakati, hivyo kila halmashauri ipange mipango yake kupitia Maafisa Elimu kata, watendaji wa kata Vijiji pamoja na Walimu kufuatilia Wanafunzi wote wanaripoti shule wasisubiri agizo la RC au DC la kwenda kuwasaka kwa kuwa mifumo ipo, na kuhakikisha wanafunzi wote wamepatikana" Amsema
Aidha, amewasisitiza pia kuhakikisha upatikanaji wa chakula shuleni, na kuwataka kuweka mikakati ya wanafunzi kupata chakula cha mchana na kuwasisitiza Mafisa Elimu kufuatilia kwa karibu shule zilizopo kwenye maeneo yao, zinakuwa na mpango wa kutoa chakula kwa Wanafunzi kwa kuwa chakula kinaongeza ufaulu hivyo wakabuni mkakati wa kupatikana chakula.
Ameiagiza halmashauri ichague shule 10 za mfano na kuhakikisha shule hizo zinakuwa na ufaulu uliotukuka na Kila halmashauri ibuni mkakati wa kuhakikisha ufaulu wa mitihani ya taifa unakuwa ni asilimia 100%.
Kuhusu ,utekelezaji wa miradi ,mkuu huyo wa Mkoa,amezitaka halmashauri za Wilaya kuhakikisha zinazingatia miongozo ya kukamilisha miradi yote ya Ujenzi kwa wakati na ubora na Serikali imetoa fedha nyingi za kujenga shule hizo.
Kila halmashauri zihakikishe Elimu inayotolewa ni bora hivyo kila mmoja ajitume awe mkereketwa wa Elimu na awe na maono ya Elimu kwenye eneo lake
Kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu,mkuu wa mkoa,amesema jumla ya Wanafunzi 45908 waliohitimu elimu ya msingi mwaka jana na kupangiwa shule za sekondari za Serikali walioripoti ni 33915 sawa na asimia 74%.
Amesema Mkoa umefanikiwa kutekeleza miradi yote ikiwemo ya fedha za COVID 19,Boost ,Tozo,Uhuru umekamilika vizuri ,pia Mkoa unatekeleza miradi mwingine ya SEQUIP ,BARRICK bado inaendelea kukamilishwa kwa fedha za Serikali
Amesema uandikishaji Wanafunzi darasa la awali umefikia 55414 ,kati ya maoteo ya kuandikisha Wanafunzi 69 174 sawa na asilimia 80
Aidha uandikishaji darasa la kwanza umefikia 60378 sawa na asilimia 97% kati ya maoteo ya kuandikisha Wanafunzi 62307.
Kwa upande wake rais wa Umoja wa Wakuu wa shule za Sekondari TAHOSA ,Mwl Denis Otieno ambae pia ni mkuu wa shule ya sekondari Ilboru,amesema Wakuu wa shule wanatekeleza malengo ya Elimu ambapo wanazifanyia kazi changamoto na kuzifanya ziwe ni fursa.
Amesema changamoto iliyopo ni utoro wa wanafunzi hivyo wanashirikiana na Viongozi wa Serikali kuwafuatilia wanafunzi,na kuhamasisha wazazi kuchangia chakula .
Katibu wa TAHOSA mwl Justini Mtongi ,ambae ni mkuu wa shule ya sekondari King'ori,amesema kuwa mkakati uliopo ni kuzijengea uzoefu shule ambazo hazifanyi vizuri kwa kuzingatia miongozo mbalimbali
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa