Serikali ipo tayari kukaa na wadau wa taasisi za kibenki ili kuona namna ya kuboresha huduma za kibenki hususani riba katika mikopo.
Yameelezwa hayo na Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Chemba alipokuwa akifungua mkutano Mkuu wa 26 wa wanahisa wa benki ya CRDB, Jijini Arusha.
Amesema riba imekuwa kikwazo kikubwa kwa wananchi kushindwa kuchukua mikopo ya kufanyia maendeleo mbalimbali.
Riba kwenye mikopo ya watumishi pia imekuwa kikwazo kikubwa kwani mabenki mengi yanatoza riba ya juu na kuwaogopesha watumishi wa serikali kuchukua mikopo hiyo, ingali wao wanauhakika wakurudisha mikopo hiyo kutokana na dhamana ya ajira zao.
Aidha , Mhe. Mwigulu amesema serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya hi umuhimu wa kuwekeza katika hisa kwani ndio uwekezaji wenye uhakika zaidi.
Wananchi wengi hawana uwelewa wa kutosha juu ya uwekezaji katika hisa ndio maana hata muamko bado upo chini sana ukilinganisha na nchi nyingine.
Pia,imeitaka Benki kuu ya Tanzani (BOT) kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi kwa mabenki kifungua matawi mengi hasa katika nchi za nje ili kuongeza mzunguko wa fedha nchini na kukuza uchumi.
Akitoa taarifa fupi ya hali ya uwekezaji nchini Mwenyekiti wa bodi ya benki ya CRDB Dkt. Ally Ally amesema, takribani watanzania 700,000 ndio wamewekeza katika hisa sawa na asilimia 1.25.
Aidha, Dkt Ally ameipongeza benki hiyo kwa kuweka mazingira mazuri kwa watanzania kuwekeza katika hisa kwani zaidi ya asilimia 80 ya hisa za benki hiyo zinamilikiwa na watanzania wenyewe.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB bwana Abdul Majdi amesema, benki hiyo imekuwa miongoni mwa benki zinazofanya vizuri katika soko la hisa kwa sababu serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji.
Kwa sasa hisa moja ya benki hiyo inanunuliwa kwa shilingi 290 kutoka shilingi 95 kwa mwaka 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella ameipongeza benki ya CRDB kwa kuamua kufanya mkutano huo katika Mkoa wa Arusha kwani wangeweza kufanyia Mkoa wowote lakani wakachagua Mkoa wa Arusha.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa