Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Paul Christian Makonda ametangaza kuongezeka kwa madaktari wengine 100 na kufikia wahudumu wa afya 550 kutoka idadi ya wahudumu wa afya na madaktari 450 waliokuepo hapo awali, na kusiitiza kuwa lengo ni kuongeza kasi na ufanisi katika kuwahudumia wananchi wenye uhitaji wa matibabu, vipimo pamoja na dawa.
Aidha Mhe. Makonda pia ametangaza kuongeza vitenganishi vya maabara pamoja na mahema ya kudumia wananchi kutokana idadi kubwa ya watu wanaojitokeza kila uchao kwaajili ya kuhudumiwa kwenye kambi hiyo.
Mhe. Makonda pia ametangaza uwepo wa wahudumu wa afya na madaktari wanafunzi takribani 25 kutoka nchini Marekani ambao wamefika kwenye kambi hiyo ya Matibabu pamoja na uwepo wa kamati maalum ya rufaa itakayosimamia safari za wagonjwa watakaobainika wanahitaji matibabu ya ziada kwenye hospitali za kanda na Taasisi za afya.
"Ninawatangazia wananchi wote kuwa tumeandaa utaratibu mpya wa kuhudumia makundi maalum ya wazee, watoto na aki mama wajawazito ili kuwaepusha kukaa muda mrefu kwenye misururu" Amesema
Kaulimbiu ya Kambi hii ya madaktari bingwa ni "Afya yako mtaji wako, kazi yetu ni kukupatia huduma bora"
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa