Na. Elinipa Lupembe
Maafisa Tarafa na Maafisa Watendaji wa kata wameaswa kuwajibika katika kutekeleza majukumu yao kwa kuibua miradi ya maendeleo kutokana na fursa zilizopo kwenye maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo endelevu vya Mapato na kuvisimamia.
Rai hiyo, imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa, wakati wakati akifungua mafunzo kwa Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata Mkoa wa Arusha, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano kwenye Ukumbi za Mikutano Ofisiya Mkuu wa mkoa huo
Amewasisitiza Watendaji hao kuwa wabunifu wa vyanzo vya mapato ya Serikali na kuhimiza uwajibikaji wa watumishi na ushiriki wa wananachi katika maendeleo.
“Mara nyingi tunate tumekuwa hatuna ubunifu wa usimamizi na uwajibikiaji, tuna fursa nyingi za kiuchumi lakini hatuna ubunifu, hatusimamii, fursa za kijamii zinazopatikana kule hatuzielezei vizuri” alisema Bw. Missaile Musa.
Amesema uwepo wa changamoto zinazotokana na kutozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika utendaji wa watendaji hao katika ngazi ya msingi, zitapata suluhu baada ya mafunzo hayo hususani masuala ya maadili, uzalendo na masuala ya kiutumishi.
Aidha, amewataka kutambua majukumu yao kwa kina ili kuepuka muingiliano wa kimajukumu na kimaslahi, zaidi kufahamu masuala ya kisera na kuhimiza utekelezaji wake huku akiwataka Watendaji Kata kuandaa Mpango kazi wa Kata na kabla haujawasilishwa ngazi ya Halmashauri lazima upitie kwa Afisa Tarafa wake ili kuwa na agenda ya pamoja katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa upande wa Afisa Mtendaji wa Kata ya Naikanuka, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ,amesema mafunzo hayo yatamwongezea weledi wa kazi na kuboresha ushirikiano na watumishi wa Sekta zote katika eneo lake yeye akiwa kiungo muhimu Pamoja na kuweza kutatua kero na migogoro ya wananchi kabla ya viongozi kufanya ziara katika eneo lake.
Awali, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, amebainisha kuwa mafunzo hayo ya siku mbili yanatolewa na ofisi hiyo, kupitia Programu ya Uimarishaji wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na vyuo vya Serikali za Mitaa Hombolo na Chuo cha Utumishi wa Umma, kikiwa na washiriki 181, Watendaji wa Kata 157 na Maafisa Tarafa 23 kutoka Tarafa na Kata zote za Mkoa wa Arusha.
Hata hivyo, ameweka wazi kuwa, awamu hii ya mwisho itahusisha mikoa ya Arusha, Iringa, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Morogoro, Tanga na Ruvuma, ambapo Maafisa Tarafa 203 na Watendaji wa Kata 1,377 watapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa