Wakati anakabidhiwa Ofisi tayari kuanza Majukumu yake mapya kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Paul Christian Makonda alitaja vipaumbele sita anavyokuja kushughulika navyo mkoani Arusha.
Moja kubwa lilikuwa kuweka msingi wa Haki, akisema asipokuwa Kiongozi wa Kutenda haki, hatokuwa akiwakosesha haki watu wa Arusha pekee, bali yeye pia na uzao wake.
"Wananchi wanaodhulumiwa, wanaonyanyaswa, wanaochelewesgwa na kuzungushwa kupata haki zao nimekuja kusimama kwa niaba yao, kama mtu yupo Ngaramtoni, Monduli wapi Popote alipo iwe Arumeru, ili mradi una haki yako na unajua ni haki yangu, sitajali hujasoma, huna pesa, sitajali kama una ndugu mwenye mamlaka, nitasimama kwenye nafasi yangu kuhakikisha unapata haki yako." Alisema Mhe. Makonda Aprili 08, 2024.
Leo Mei 08, 2024 Umati wa watu umejitokeza kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, tayari kuzungumza na kusikilizwa changamoto zao mbalimbali kwenye Programu maalum ya siku tatu ya Mhe. Mkuu wa mkoa ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Mkoa huu.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa