Maofisa Habari na mawasiliano nchini wametakiwa kuelewa dhana nzima ya akili hisia na namna ya kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo sehemu za kazi na katika familia.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa mwaka wa Chama cha Maofisa Mawasiliano Serikalini unaofanyika kwenye ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Prof. Gabriel amesema kwamba dhana ya akili hisia hivi sasa imeanza kupata kasi kwenye ngazi ya Serikali hivyo inasaifia ni namna gani unaweza kufanya kazi pamoja na kuwajibika sehemu ya kazi.
“Watu wa Mawasiliano mna umuhimu mkubwa sana katika dhana hii kwani inawasaidia muwasiliane vipi na watu”.
Aidha, alisema ni vyema kuweka mazingira mazuri sehemu ya kazi na kwenye maisha yao ya kawaida kwa familia kwani muda zaidi ya 90% ya maisha yao wanayatumia kazini
“Ni lazima mjitahidi kukabiliana na changamoto katika majukumu yenu na hata katika familia zetu ,pia epukeni kuwa chanzo cha msongo wa mawazo kwa watumishi wengine ili isiwaletee tatizo katika afya zenu”.
Hata hivyo amewataka maofisa hao kuwasaidia viongozi na jamii inayowazunguka kuzuia akili hadi ili isiwaletee madhara katika utendaji wao wa kazi wa kıla siku
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa