Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Doto Biteko , amewahimiza viongozi na watumishi wa Umma waliopewa dhamana na Serikali kuwahudumia wananchi kikamilifu huku akisisitiza kuwa uhalali wa Serikali yoyote ya kidemokrasia duniani imelenga katika misingi ya kuwatumikia wananchi na si vinginevyo.
Dkt. Biteko ametoa rai hiyo, wakati akifungua Kongamano la 15 la Watalaamu wa Ununuzi na Ugavi, linalofanyika Jijini Arusha kwenye kituo cha Kimataifa cha Mataifa Arusha, mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Paul Christian Makonda, kuwasifu wakazi wa Kata ya Muriet Jijini Arusha, walioamua kumburuza Diwani wao kwenye Matope kama sehemu ya kuonesha hisia zao za kukerwa na ubovu wa barabara nyingi za Kata hiyo na hivyo kusababisha adha nyakati za misimu ya mvua kwa muda mrefu sasa.
"Huwa ninashangwazwa kiongozi kusimama kwenye msiba na kujitambulisha yeye ni kiongozi wao, wakati wananchi wanakabiliwa na kero na changamoto nyingi za kijamii katika eneo lao, viongozi tunatakiwa kujitathmini na kuitambua dhamana tuliyopewa ya kuwahudumia wananchi katika maeneo yenu kama mlivyowaomba kuwachangua" Amesisitiza Dkt. Biteko.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa