Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili Mkoani Arusha kupokelewa na wenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdini Babu na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro jioni ya leo Novemba 27,2024.
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yupo Mkoa wa Arusha, kwa ziara ya Kikazi ya siku nne, pamoja na mambo mengine, Dkt. Samia kesho Novemba 28,2024 anatarajiwa kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi katika chuo cha mafunzo ya Kijeshi Monduli, kushiriki kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki pamoja na kuwa na mkutano na Viongozi wa jamii ya Kimasai mkoani Arushmk
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa