Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Jumapili ya Disemba Mosi, 2024 anatarajiwa kuwa Jijini Arusha, kuzungumza na Viongozi wa Jamii ya kimasai wanaoishi Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha ili kuwasikiliza na kujadiliana kwa pamoja kuhusu changamoto za Jamii hiyo ndani ya Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumapili Novemba 17, 2024 wakati akitoa tathimini ya utendaji wake kwa miezi sita ya awali, akiisifu Jamii ya kimasai kwa usikivu na utulivu wao wakati serikali ilipokuwa inashughulikia mgogoro baina yao.
Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ni eneo la urithi wa dunia likiwa linakaliwa na mifugo, wanyamapori na binadamu ambapo mgogoro mkubwa wa sasa ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na athari zake kimazingira suala ambalo limesababisha mgawanyiko kwa wale waliokubali kuhama katika eneo hilo na wale wasiiona tatizo kwa wao kuongezeka idadi yao ndani ya mamlaka hifadhi hiyo ya wanyamapori.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa