• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RAIS SAMIA NURU YA WATOTO LAKE EYAS KARATU;AJENGA SHULE YA SEKONDARI......

Posted on: October 25th, 2023


Na Elinipa Lupembe


Eneo la lililozunguka ziwa Eyas maarufu kama Lake Eyas kijiji Langhangareni kata ya Mango'ola wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha, liko umbali wa takribani Km 67 kutoka makao makuu ya wilaya, ni takribani mwendo wa zaidi ya saa moja kwa gari.


Katika hali isiyo ya kawaida kwa wananchi wa kijiji cha Langhangareni, Serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kujenga shule mpya ya sekondari, kwa gharama ya shilingi milioni 584.2 kupitia programu ya kuboresha miundombinu ya shule za sekondari nchini ( SEQUI)


Wananchi hao wamemshukuru Rais mama Samia Suluhu Hassan, kwa kuona umuhimu wa kijiji chao kuwa na shule, kwa kuwa watoto wao sasa watasoma sekondari kama ilivyo kwa watoto wengine wa kitanzania.


Wamesema kuwa watoto walitembea umbali wa zaidi ya Km 22 kwenda na kurudi shule, wakisoma shule ya sekondari Domel iliyopo Mang'ola Barazani zaidi ya Km 11, hali ambayo ilisababisha watoto wengi kukata tamaa na kuacha shule huku wasichana wakitumbukia kwenye ndoa za utotoni.


Abdala Rashidi ameonesha furaha yake wazi kwa kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwekeza fedha nyingi ambazo zinakamilisha ujenzi wa shule tofauti na hapo awali zililetwa fedha za kujenga darasa moja moja, na kusisitiza kuwa maendeleo ya Serikali ya mama Samia yanakwenda kwa kasi kubwa.


"Haijawahi kutokea kijiji chetu kupata mamilioni ya fedha, huku ni mbali sana lakini mama Samia ametuona na ametuthamini, majengo mazuri kama shule za mjini, watoto wetu sasa hawatasoma mbali, na tutahakikisha wote wanakwenda shule"Amesisistiza Rashidi


Naye Swai Kuzali, amethibitisha kuwa yeye binafsi hakupata nafasi ya kupata elimu ya sekondari, kutokana na mazingira ya shule kuwa mbali sawa na vijana wengine wa kijiji hicho cha Laghangareni na kuahidi kuhakikisha watoto wake wanatumia fursa hiyo kusoma ili kuwa na watalamu kutoka katika  kijiji chao.


"Mimi sikusoma sekondari shule ilikuwa mbali, ilitukatisha tamaa, vijana tuliamua kuingia kufanya shughuli za kilimo na uvuvi  tunafuraha kwa kuwa  watoto wetu watasoma, kijiji chetu kitakuwa na watalamu kama maeneo mengine, Mama Samia kaleta mapinduzi Langhangareni" Amesisitiza Kuzalia


Ikumbukwe kuwa ujenzi wa shule za sekondari ni utekelezaji wa Ilani yaCCM 2020 kuelekea 2025 Ibara ya 80 kifunga (a) Kujenga na kukarabati miundombinu ya elimu pamoja na kuhifadhi

na kuendeleza mazingira ya shule hizo


#arushafursalukuki

#KaziInaendelea

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa