Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Arusha Mwl.Tumsifu Mushi amemkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Albano Musa, Tuzo ya Heshima kwa Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Kwa niaba ya walimu na Wadau wa Elimu Mkoa wa Arusha, ikiwa ni kutambua na kuthamini mchango wake mkubwa kwenye sekta ya Elimu katika Mkoa wa Arusha, mapema leo Septemba 17,2025.
Wadau hao wa Elimu wamekabidhi tuzo hiyo wakati wa Kongamano la Wadau wa Elimu kuelekea Juma la Elimu, Konga lililowakutanisha viongozi wa elimu, walimu, wanafunzi na wadau wa elimu mkoa wa Arusha likiwa na lengo la kusherehekea mafanikio ya sekta ya elimu katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Hata hivyo ameahidi kufikisha tuzo hiyo kwa Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassani.
Kauli mbiu ya Kongamano hilo ni "Elimu Bora na Miundombinu Bora ni Msingi wa Arusha Mpya na Tanzania yenye Maendeleo Endelevu"
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa