• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC KIHONGOSI AKABIDHIWA OFISI..

Posted on: July 1st, 2025

Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha, Mhe.Kenan Laban Kihongosi, amekabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda na kuanza kazi rasmi na kuhudhuriwa na viongozi wa Chama na Serikali, watumishi wa Umma, viongozi wa dini na mila, pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo, mapema leo mapema leo Juni 30, 2025.

Hafla hiyo ilianza kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu na shughuli za utekelezaji wa mkoa huo huku akieleza mafanikio yaliyopatikana kisekta kwa kipindi chote alichohudumu.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu mpya wa Mkoa Mhe. Kihongosi, amemshukuru Mwenyenzi Mungu  kupitia Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan kwa imani yake kubwa na kumpa dhamana ya kuongoza  Mkoa wa Arusha na kumshukuru Mtangulizi wake Ndugu Makonda kwa kazi kubwa aliyoifanya katika mkoa huo, kazi ambayo ameacha alama kubwa mkoani hapo.

"Mhe.Rais amenituma Arusha kuja kuwatumikia wananchi wa Arusha na nimekuja kufanya kazi, ninachoomba kwenu ni ushirikiano ili kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo, tukiwa na lengo la kuhakikisha wananchi wa Arusha wanafurahia matunda ya nchi yao". Ameweka wazi Mhe.Kihongosi

Aidha, amesisitiza kutoruhusu kikwazo chochote kitakachozuia agenda ya maendeleo katika utendaji kazi, wajibu wake ni kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiweo matumizi sahihi ya fedha za Umma zinazoletwa kwa ajaili ya kutekeleza  miradi ya maendeleo.

Tutakutana site, tutafanya ziara wilaya zote,  tutakagua miradi ya maendeleo, tutasikiliza na kutatua kero za wananchi,  Hatutamuacha mtu nyuma, kwa kuzingatia huu ni mwaka wa uchaguzi, Viongozi bora wakatambulike kwa zilizofanywa na serikali". Amesema

Zaidi amewataka watumishi wa Umma kufanya kazi kwa weledi na uadilifu kwa kusimamia Kanuni, Sheria na taratibu kwa kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi wote, ili  kila mtua aweze kufurahia matunda ya Serikali na Nchi yake.

Awali Mhe.Kihongosi amehamishiwa mkoani Arusha akitokea Mkoa wa Simiyu kufuatia mabadiliko ya uongozi yaliyofanywa na Mhe. Rais na kuagizwa kuja kuwaaunganisha wanaArusha.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO MTIHANI WA UTAMIRIFU (MOCK) 2025 DARASA LA SABA (VII)- MKOA WA ARUSHA June 07, 2025
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKALLA: UFUNGUZI TAWI LA CRDB NAMANGA UTACHOCHEA BIASHARA NA UCHUMI WA WANANCHI WA MPAKANI ..

    September 26, 2025
  • RC MAKALLA ATAKA MPANGO MKAKATI WA UTALII UKIJUMUISHA FURSA NA MAANDALIZI YA AFCON 2027...

    September 25, 2025
  • WANANCHI WALIOLALAMIKIA MGAO WA MAJI WAFURAHIA UJENZI WA TENKI JIPYA LA MAJI...

    September 24, 2025
  • RC MAKALLA: ARUSHA ITAENDELEA KUWA NA AMANI SASA NA HATA  BAADA YA UCHAGUZI...

    September 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa